Posts

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA

Image
Mwanamuziki tokea pwani ya Kenya,P-day ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya mauaji ya wazee wanaoshukiwa kuwa wachawi pande za Kilifi. Msanii huyo aliyetamba kwa kibao tarumbeta,Nylon guitar,Visingizo,Niringe naye na vinginevyo amedokeza haya kupitia ukurasa wake wa facebook akikashifu vikali vitendo hivyo. P-day alisema ya kwamba usemi wake anaopenda kuusema kwa nyimbo zake....."MZEE HATEMEWI MATE" unapaswa kuwa kauli mbiu itakayochukuliwa na kuwekwa kama mtajo utakaowaokao wazee kutoka kwenye janga hili. Tukinukuu kutoka alichonakili kwenye akaunti yake ya facebook..... "Social cohesion department to buy the mzee hatemewi mate lebol ( uzee si uchawi ) nliamka tu nkatunga hii lebol din't know itafika huku ........Sasa vijana kilifi county walianza kuua wazee kwa kua niwachawi BT sio Kila mwenye mvi ni mchawi ..let's respect the old" JE MAONI YAKO NI YAPI KUHUSIANA NA PENDEKEZO LA P-DAY KUHUSIANA NA WAZEE KUUAWA?

FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY

Image
FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY PWANI USANII:HARUN DEEY NI NANI HASWA? HARUN : Harun Iddy almaarufu Harun Deey alizaliwa 22/02/1997 na nilianza muziki alnikiwa na umri wa miaka kumi na sita. PWANI USANII:NYIMBO YAKO YA KWANZA ILIKUA GANI? HARUN: NASUBIRI ndiyo iliyokuwa nyimbo yangu ya kwanza ikifuatiziwa na NYOTA, zote nilizifanya Liwazo records,Mombasa. PWANI USANII:LABDA ULIANZA KUPATA UFANISI LINI KWENYE TASNIA YA MUZIKI? HARUN: Nilianza kupata ufanisi kupitia kwa wimbo wangu wa tatu unaojulikana kama BOSS DON ulioniwezesha kupata show kwenye vilabu tofauti vikiwemo HYPNOTICA (VIPAJI NIGHT), Z LOUNGE (XTRAVANGANZA NIGHT) na DANS LOUNGE (CELEBRITY THURSDAYS). Vilevile siwezi upuuzia wimbo wangu unaojulikana kama MAJARIBU manake ndio ulionipatia video yangu ya kwanza. PWANI USANII:JE VIDEO YA MAJARIBU ILIFANYA VYEMA AMA? HARUN: Ndio ilifanya vyema,iliweza kuchezwa kwenye Y254'S PWANI SHOW,Y IN THE MORNING,KBC na RAIA TV. PWANI USANII:NYIMBO

MSANII MKUBWA WA PWANI AGEUKA KUWA MGANGA HATARI!!!!!!

Image
Ni habari motomoto na za kutamausha zilizofikia meza yetu ya habari hivi majuzi. Msanii chipukizi anayetokea mtaa wa Mbandi,gatuzi dogo la Kinango amewashangaza wengi pale alipoupiga teke usanii wake kwa muda na kujiunga na uganga. Msanii huyo chipikuzi anayejulikana na wengi kama Boss Michapo amekua mganga sifika guku akivutia wateja wengi kutoka kanda yote ya pwani. Michapo amekua akivuma kwa vibao motomoto vinavyopigwa sana kwenye madisko vumbi na disko matanga. Ilifikia wakati msanii huyo alipogonjeka na kwenda nchi jirani ya Tanzania kutibiwa ndipo aliporudi na kuwa mganga hodari. Inakisiwa kuwa Boss Michapo alienda Bongo na kununua mkoba wa uganga. Hivi sasa msanii huyu huenda studio na kulipia wasanii wenzake wamuandikie nyimbo kwa sababu hana muda wa kukaa chini na kuandika nyimbo. Jamaa huyu vilevile amesema hivi karibuni atasifika Afrika Mashariki yote kwa kuwa amepanga vibao motomoto na atatumia nguvu zake za kiganga kupenya kwenye soko la muziki. Vilevile amewakaribishw

MSANII SHEPHARD KAMFANYA NINI PROMOTER WAKE LUKESMART ?

Image
BAADA YA PURUKUSHANI ,JE MSANII SHEPHARD KARUDIANA NA PROMOTER WAKE LUKESMART ENTERTAINMENT???? Ni mnamo mwezi wa saba pale vute nikuvute zilitanda kati ya msanii Shephard na promota wake Lukesmart. Baada ya Lukesmart kumsimamia Shephard kwenye project zake kadhaa na kuandaa tamasha nyingi wawili hao walianza purukushani na malumbano hadi ikapelekea uhusiano wao wa kikazi kuvunjika. Ni hivi majuzi tu baada ya Shephard kutoka safari zake za Zanzibar na Tanga ambapo Shephard alipost picha akiwa na promoter wake wa zamani Lukesmart. Vilevile si muda mrefu tayari Shephard akadondosha kibao kipya akimshirikisha Dazlah kwa jina 'CHEKO'. Tazama hapa - >https://youtu.be/O-Tdf6XmCSU

MASAUTI APAZA SAUTI ZAIDI GAGA

Image
MASAUTI APAZA SAUTI ZAIDI Ali Mohamed Said,almaarufu Masauti amepaza sauti kwa mara nyingine tena. Msanii huyu aliyetamba kwa vibao kadha wa kadha vikiwemo Mahabuba,Nurulain na vinginevyo alitudokezea kuhusu kazi yake mpya Gaga. Wimbo huo unaozungumzia tamaa ya kumtongoza binti mwenye hadhi ya juu umeyaleta mawazo yake msanii huyu aliyeandaa wimbo wake chini ya producer Motiff. "Video ya wimbo Gaga ipo tayari na iliandaliwa Mombasa na vilevile Nairobi,hivi karibuni itawachiliwa rasmi." Alitudokezea Masauti. Kupitia meza yetu ya habari,msanii huyu yupo katika safari ya kuiteka Afrika Mashariki kwa vibao motomoto alivyovitayarisha na atavidondosha tu pindi wakati murwa utimiapo. Kwa sasa tazama video yake ya awali....NURULAIN --- > https://youtu.be/8gIsxa3uEYA

SIJAWACHA MUZIKI BAADA YA HARUSI MSANII SHEPHARD APASUA MBARIKA

Image
SIJAWACHA MUZIKI BAADA YA HARUSI,MSANII SHEPHARD APASUA MBARIKA. Msanii Shephard amevunja ukimya wake baada ya kufunga harusi na kwenda chini ya maji. Shephard wa kibao kikali cha 'mdogo mdogo' kupitia mahojiano ya njia ya simu amedokezea meza yetu ya habari kwamba baada ya harusi alienda fungate (honeymoon) na mkewe kama inavyotakiwa. Msanii huyu aliongezea kuwa kwa sasa ameshajitayarisha kimuziki na tayari yupo na kibao kipya kwa jina 'cheko'. Kibao hiki amekitayarisha chini ya produza Tee wa Tee Hits productions. Video yake imefanywa na Director Nezzoh Monts na punde si punde atawachilia mzigo. Kaa mkao wa kula,usicheze mbali !!!

SINA HAJA NA VINYAGO VYA TUZO ZA KENYA COAST MUSIC AWARDS DJ IVORY AFOKA

Image
DJ IVORY AZIKASHIFU NA KUTUPILIA MBALI TUZO ZA KENYA COAST MUSIC AWARDS 2018. Deejay sifika Kenya anayetokea pwani,Dj Ivory amekashifu vikali tuzo za KCMA 2018. Tuzo hizi zinazoongozwa na CEO Beyonce wa kampuni ya Beyonce promotions zinawaleta bayana wasanii hasa wa hapa pwani kuwania vitengo tofauti tofauti vya sanaa. Ivory kupitia mtandao wa facebook alijitoa kwenye kinyanganyiro hicho na kukashifu vikali dhidi ya tuzo hizo akisema ya kuwa hazina manufaa yoyote pasi na kupewa vinyago tu visivyo na faida. Tukinukuu alichonakili hapa........ " Let me respond to beyonce and her team for saying certain people have grown too cool for awards. We've grown from sculptures to understanding that majority of these awards in our region are bullshit. What has that award brought all through the years apart from not paying performers big debts and leaving Most Artist most Artist Stranded no tickets back no hotel accommodation. We know you and we've been there. I dont wann